Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao Hill PCO, Tebby Yoram alisema kuwa shamba hilo lina miti ya asili ambayo imekuwa kivutio cha utalii.
Utalii wa mbio za magari katika shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa lilivyovutia watu wengi 
Sehemu moja wapo wa shamba la miti Sao Hill ambalo limekuwa kivutio cha watalii 


Na Fredy Mgunda, Iringa.

UONGOZI wa shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa unawakaribisha wananchi kufanya utalii hilo kutokana kuwa na maeneo muhimu kwenye shamba hilo ili kuongeza mnyororo wa thamani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao Hill PCO, Tebby Yoram alisema kuwa shamba hilo lina miti ya asili ambayo imekuwa kivutio cha utalii.

PCO Yoram alisema kuwa wamekuwa wanahamasisha utalii wa ikolojia kwa wadau mbalimbali wa utalii kutembelea vivutio vilivyomo katika shamba la miti Sao Hill.

Alisema kuwa kuna utalii wa matembezi,kuona viumbe mbalimbali,utalii wa ufugaji nyuki,utalii wa michezo mbalimbali kwa kuwa shamba hilo limekuwa na barabara zilizotengenezwa vizuri kwa ajili michezo ya magari, baiskeli na kutembea kwa miguu.

PCO Yoram alisema kuwa wameshafanya mara tatu utalii wa michezo ya mbio za magari na umeleta mafanikio makubwa kwa kukusanya maelfu ya wadau wa utalii wa mchezo wa magari hivyo wananchi na wadau wa utalii wanaombwa kuendelea kwenda kufanya utalii katika shamba la miti Sao Hill.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: