Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao, ambapo amesema miongoni mwa watu wanaoshikiliwa yupo kinara ambaye ni kiongozi wa mtandao wa ‘vishoka’ mkoani humo.

“Tumeshakamata kiongozi wao mkubwa wa hicho kikosi ambaye amekuwa akishirikiana na mtandao mkubwa ambao upo ndani ya watumishi hawa wa Tanesco, wote hawa tumewakamata na tuko kwenye hatua nzuri,”alisema Kamanda Maigwa

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori alisema watu hao wamekuwa wakiihujumu serikali kwa manufaa yao wenyewe na kuikosesha serikali mapato yake.

Aliendelea kusema mpaka sasa watu 21 maeneo ya Kibosho , wilayani humo wamefungiwa umeme kinyume na taratibu na kila mwananchi ameunganishiwa umeme kwa kulipishwa Sh400, 000 na kwamba fedha hizo haziingi serikalini.

“Jambo hili tumeligundua katika kata yetu ya Kibosho, hawa watu walikuwa wanaenda kuwaunganishia wananchi umeme kwa utaratibu ambao haufahamiki ndani ya shirika, hii ni kuihujumu serikali na kuikosesha mapato.”

DC Makori Amesema hii ni hatari hata kwenye usalama wa wananchi kwasababu watu waliokuwa wakifanya hujuma hii hawakuwa wakifanya kwa kufuata utaratibu wa kisheria na wa kitaalamu, nalipongeza Jeshi la polisi kwa hatua kubwa ambazo wameendelea kuchukua dhidi ya jambo hili na kushughulikia kwa weledi,

DC Makori Aliendelea kusema baada ya kupata taarifa ya watu hao kuihujumu serikali kulifanyika operesheni kubwa katika wilaya hiyo, na jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata mtandao wa watu hao katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

“Nalipongeza sana Jeshi la polisi kwa kazi kubwa waliyofanya ya kufanikisha jambo hili, Polisi wamefanyika kazi kubwa ya kubaini na kukamata mtandao huu ambao ulikuwa ukihujumu miundo mbinu ya umeme,”

DC Makori alisema baada ya upelelezi kukamilika watu hao watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwabaini watu hao ambao sio wazalendo kwenye taifa hili.

Mbali na hayo yote Dc Makori ametoa onyo kali kwa watumishiri wa Serikali ambao wanashiriki kuhujumu mali na miundombinu ya Serikali ambayo Amesema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani anapambana usiku na mchana kutengeneza na kuleta Maendeleo chanja kwenye Taifa letu, auto mvumilia yoyote yule atakaye hujumu Serikali hii

Alipotafutwa Meneja wa Tanesco mkoani hapa, Grace Ntungi kuhusiana na kukamatwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo , alisema hawezi kuzungumia suala ambalo lipo kwenye upelelezi na kwamba viachiwe vyombo hivyo viendelee na kazi yake.

“Hizi taarifa zipo chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi, taratibu za uchunguzi zitakapokamilika tutatoa pia taarifa, ili tusije vuruga taratibu za Jeshi letu la polisi.”alisema Meneja huyo.

Share To:

Post A Comment: