BAADA ya kutinga katika hatua ya 16 bora michuano ya Kombe la Azam Sports Federatio (ASFC) Timu ya Tabora United kesho itashuka tena katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara dhidi ya Singida Big Stars .
Mchezo huo ambao utapigwa saa nane kamili mchana (14:00), wachezaji wa Tabora United chini ya kocha Mkuu Goran Copnovic wamefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuzisaka alama tatu muhimu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Nyuki hao watabora wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo wa kesho ili kuendelea kujitoa kwenye nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu na hivyo kumaliza kwenye nafasi nzuri wa msimamo mwisho mwa msimu wa mwaka huu 2023/2024.
“Tunakwenda kwenye mchezo wa kesho tukifahamu kuwa pamoja na kwamba tutakuwa nyumbani lakini mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila mmoja wetu kuhitaji matokeo ya ushindi kwa maana ya alama tatu muhimu, lakini kama Timu tumejipanga kuwapa furaha mashabiki zetu, hivyo wasiwe na wasi wasi.
Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wapo vizuri, wanahari na morali na kwamba hakuna mchezaji mwenye changamoto yoyote ya ki Afya hivyo mashabiki watarajie kupata burudani nzuri kutoka kwa vijana wetu”.
Tabora United itashuka kwenye mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare dhidi ya Azam FC katika mchezo wa kwanza mzunguko wa pili uliopigwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Februari 19 na hivyo kusogea hadi kwenye nafasi ya 13.
Share To:

Post A Comment: