Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ametoa miezi mitatu kwa wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Maguhungwa Kata ya Mwakata,Halmashauri ya Msalala,Wilayani Kahama kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu na baada ya miezi hiyo kumalizika watatakiwa kuondoka kwa hiyari bila kusukumwa.

 

Hatua hiyo imekuja kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya wachimbaji wadogo ,wamiliki wa mashamba na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya CANUCK ambao ndio wenye leseni ya uchimbaji kwenye eneo hilo.

Naibu waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa amesema wameruhusu duara hizo kufunguliwa kwa kipindi cha mpito wakisubilia ofisi ya afisa madini kutafuta maeneo ambayo yatawasaidia kuendelea na shughuli zao za uchimba,huku akielekeza kwa kampuni hiyo kutoa kipaumbele kwa kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo hayo.

 

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi,amemuomba Naibu waziri wa madini kuhakikisha leseni ambazo watapatiwa wananchi wapewe zile ambazo zinauzalishaji wa madini. zitakazowasaidia kupata dhahabu.

Share To:

Post A Comment: