NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

SOKO la Mbuyuni manispaa ya Moshi  mkoani Kilimanjaro limeteketea kwa moto na kuacha wafanyabiashara zaidi ya 2500 wakiwa hawajui la kufanya baada ya bidhaa zao zote kuteketea.

Moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na chanzo chake bado hakijajulikana,umesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao ambao asilimia kubwa wanaendesha biashara kwa mikopo.

Aikizungumza mara baada ya kutembelea soko hilo na kujionea hasara hiyo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), na Mjumbe wa Kamati Kuu  ya CCM (MCC), Rabia Abdallah Hamid alisema kuwa, chama cha Mapinduzi kitaenda kuongea na taasisi za benki ambazo zimewakopesha wafanyabiashara wa soko hilo kuhakikisha hawanyanyasiki katika kurudisha mikopo yao.

“Viongozi mnapaswa muanze mara moja kuwatambua ni wafanyabiashara wangapi ambao walikuwa na mikopo na asiachwe hata mmoja kwani kunautaratibu wa kurejesha marejesho kila mwezi lakini kwenye hili sisi chama cha Mapinduzi tutaenda kukaa na taasisi hizo ili kuhakikisha wafanyabiashara hawa hawanyanyasiki katika kipindi hiki” alisema Rabia

 

 

 

 

Share To:

Post A Comment: