Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amewasili mkoani Katavi Katavi leo tarehe 19 Februari 2024 ambapo mbali na mambo mengine atashiriki Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Katika mkutano huo utakaofanyika Februari 24, 2024 katika Shule ya Sekondari Nizengo Pinda-Kibaoni Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia Nov 2020 hadi Februari 2023 itawasilishwa na Mhe. Pinda.
Mgeni rasmi katika mkutano huo utakaofanyika anatarajiwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa atazindua Radio ya Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele itakayojulikana kama Mpimbwe Fm.
Mara baada ya kuwasili mkoani Katavi Mhe, Pinda alikutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Bi. Mwanamvua Mrindoko pamoja na kutembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Katavi.
Post A Comment: