Na Abdallah Nassoro-MOI

Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wabobezi kutoka Chuo Kikuu cha Colorado cha nchini Marekani wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa Tisa wenye matatizo ya uvimbe kwenye Ubongo kwa njia ya kisasa ya kutoboa tundu ndogo bila ya kufungua fuvu katika kambi ya mafunzo ya wiki moja inayoendelea MOI jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa tatu wa kimataifa wa mafunzo ya matibabu ya kisasa upasuaji wa uvimbe kwenye ubongo yanalenga kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo madaktari bingwa wazawa, wauguzi wabobezi na wataalam wengine yamefunguliwa leo Februari, 19, 2024 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome.

“Mwaka 2017 tulianza upasuaji wa uvimbe wa ubongo bila kupasua fuvu, kwa takribani wagonjwa 572 tunawafanyia upasuaji wa vivimbe kwenye ubongo kwa mwaka, hivyo mafunzo haya itasadia uanzishwaji wa huduma mpya na tupo tayari kwa kutoa huduma mpya kwababu tunao madktari bingwa 13 w upasuaji wa ubongo, niwashukuru sana wenzetu wa Chuo Kikuu cha Colorado kwa ushirikiano huu” amesema Mchome

Mratibu wa mafunzo hayo, daktari bingwa Dkt. Nicephorus Rutabasigwa amesema katika kambi hiyo ya matibabu wagonjwa Tisa watafanyiwa upasuaji.

Kwa upande wake Prof. Ryan Ormond wa Chuo Kikuu cha Colorado amesema mkutano huo wa tatu wa kimataifa wa matibabu ya uvimbe katika ubongo ni muendelezo wa ushirikiano baina ya chuo hicho na MOI.

“Pamoja na mafunzo haya pia tumetoa msaada wa vifaa tiba na vitabu kwa ajili ya kurahisisha mafunzo kwa vitendo…tunaishukuru MOI kwa ushirikiano huu muhimu ambao unalenga kukuza tasnia ya matibabu ya uvimbe kwenye ubongo” amesema Prof. Ormond

Mwenyekiti wa matibabu ya Uvimbe kwenye Ubongo wa chuo kikuu cha Colorado Pro. Kevin Lillehei amebainisha kuwa ushrikiano huo utaiwezesha MOI kuwa kituo cha umahiri cha matibabu ya uvimbe kwenye ubongo katika ukanda wa Afrika.

Kwa upande wake Muuguzi Mbobezi wa MOI, Dorcas Magawa amesema kuwa kwa upande wao mafunzo hayo yatawasaidia kutoa huduma bora za uunguzi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uvimbe katika ubongo.

Share To:

Post A Comment: