Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imetangaza matokeo ya utafiti mbinu za kudhibiti wimbi la popo Jijini Dar es Salaam ambapo imebainisha aina tatu (3) za dawa kuonesha ufanisi sambamba na mbinu zisizo tumia dawa za kuvalisha neti miti na kupunguza vichaka/matawi ya miti maeneo ya makazi.

 

Akizungumza na vyombo vya Habari Dkt. Julius Keyyu, Mkurugenzi wa Utafiti TAWIRI amesema Taasisi hiyo imefanya utafiti kwa awamu mbili ambapo utafiti wa awali ulijikita kujua ukubwa wa tatizo, na utafiti wa awamu ya pili ulijikita kufanya majaribio ya kuwadhibiti popo katika Jiji la Dar es Salaam.

 

Dkt. Keyyu ameeleza katika kuwadhibiti Popo, majaribio yamefanyika kuanzia mwezi Mei, 2023 katika Kata ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam ambapo njia za aina mbili zilitumika ikiwemo njia ya matumizi ya dawa na njia zisizo za matumizi dawa.

 

Dkt.Keyyu amesema katika njia za matumizi ya dawa, aina tatu za dawa zimeonesha ufanisi ambapo dawa ya _Repells-All®_ ilionesha uwezo wa kuwadhibiti popo kwa siku zisizopungua 46 hadi miezi mitatu kutokana na hali ya hewa, dawa _Bat (CRP)_ ilionesha kuwadhibiti popo kwa muda wa siku 12 hadi 31 na dawa ya _Industrial Naphthalene_ ilionesha kudhibiti popo kwa siku 23.

 

Pia, Dkt. Keyyu ameeleza mbinu mbili zisizotumia dawa ambazo zimeonesha kufanya vizuri ni njia ya kuishungushia miti neti ambayo imeonesha ufanisi kwa asilimia 100% hasa katika kuwadhibiti popo kuharibu miti ya matunda na njia ya mbinu ya kupunguza miti matawi/ vichaka inaweza kudhibiti popo kwa asilimia 30% hadi 50% kuendana na namna ya upunguzaji “kama wanasayansi hatushauri njia ya upunguzaji matawi au kukata miti kwakuwa si rafiki kwa mazingira” amehimiza Dkt. Keyyu

 

Ikumbukwe, miongoni mwa madhara ya popo ni uchavuzi na uharibifu wa nyumba na vifaa, uharibifu wa mazao, usumbufu wa kelele na wakati mwingine hubeba vimelea vya magonjwa.

Share To:

Post A Comment: