Klabu  ya kitambi noma veteran, imetoa msaada wa mahitaji mbali mbali katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani Arusha. 

Msaada huo umekabidhiwa kwa watoto njiti na wamama waliojifungua ambapo wamepatiwa vitu mbalimbali ikiwemo  mafuta ya kujipaka, sabuni,na mahitaji mengine ya watoto wadogo ikiwemo kofia. 

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo muuguzi katika hospitali hiyo Elizabeth Jonas Mwadende aliwashukuru kitambi noma kwa kuguswa na kujitoa kwa ajili ya watoto hao na wamama.

"Mahitaji kwa watoto hawa njiti ni makubwa na pia wanauhitaji mkubwa wa maziwa hivyo Taasisi wengine wasisite kuja bali wawasaidie kadri wanavyojaliwa,"alisema Mwadende

Naye Msemaji wa kitambi noma Sakina Simba amesema msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia Jamii kuelekea bonanza la kimataifa linalofanyika kwa siku mbili na kuongeza kuwa wamekuwa pia wakitembelea vituo vya watoto yatima.

 Bonanza la kimataifa la kitambi noma litafanyika kuanzia leo Marchi 30 na 31 likihirikisha timu 20 kutoka ndani na nje ya nchi. 

Bonanza hilo la kimataifa la kila mwaka limeandaliwa na klabu ya veteran ya kitambi noma ya jijini Arusha litachezwa katika viwanja vinne tofauti ambavyo ni Ilboru, Sheikh Amri Abeid, St. Constantine na ISM -Kisongo. 

Kwa mujibu wa mwenyekiti wake James Rugangila, alisema sasa ni msimu wa nane wa bonanza hilo la kila mwaka.

Mabingwa watetezi mpaka sasa ni Suka Veterani.

Tanzania inashirikisha timu kutoka Tanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimanjaro, Dar-es-salaam na mkoa mwenyeji wa Arusha.







Share To:

Post A Comment: