Baraza la Madiwani halmashauri ya Wilaya ya Chemba limemchangia kijana aliyefanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne na kupata ufaulu wa Daraja la kwanza pamoja na changamoto kubwa ya umbali wa Shule ambapo alikua akitembea umbali wa kilomita 5.

Mchango huo umefanyika katika kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani February 16, 2025 kutokana na Wilaya hiyo kutofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2022 ya kidato cha nne hivyo kuongeza hamasa kwa wanafunzi wengine kuendelea kusoma kwa bidii na kuongeza idadi ya ufaulu ndani Wilaya hiyo.

Mwanafunzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Ramadhani amesema alitumia umbali wa Shule kama nafasi ya kujikumbushia Yale aliyokua akifundishwa shuleni .
“Umbali kutoka shuleni ni kilomita Tano wakati wa Asubuhi na kurudi nyumbani ni kilomita Tano pia hivyo ninachofanya ni kutumika huo umbali kujikumbushia Yale ninayofundishwa shuleni “.

Pia amesema kutokana na hali duni ya kiuchumi katika familia yao pamoja na kumtanguliza mungu ndiyo Siri kubwa ya mafanikio .

“Kingine ni kwamba niliipenda sana Shule na katika siku 360 za mwaka Mimi utakuta nimekosa zile siku zenye sikukuu za kitaifa hivyo kitu Chochote ukikipenda lazima ufanye vizuri”.

Aidha Kaimu Mkurugenzi ambae pia ni Afisa elimu amesema amefurahishwa na kijana huyo na suala lake litazungumzwa kwa kina katika kikao cha wadau wa elimu kitakachofanyika tar 2-3-2024 wilayani Chemba.

Lengo kubwa la kikao hicho itakuwa ni kupanga mikakati na mbinu Bora za kutumika ili kuinua kiwango cha ufaulu wilayani Chemba

Share To:

Post A Comment: