Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Prof. Justinian Ikingura ameitaka Menejimenti ya GST kuongeza juhudi, weledi na ubunifu kwenye utendaji kazi ili kutekeleza agenda ya Vision 2030 kwa ufanisi.

Hayo ameyasema katika Kikao cha 17 cha Bodi ya GST kilichofanyika leo Januari 19, 2024  katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma Jijini Dodoma.

Aidha, Prof. Ikingura amepokea taarifa ya Utekelezaji ya GST kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 pamoja na Rasimu ya Bajeti ya Taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pia, amepoke Taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala, Taarifa ya Kamati ya Jiosayansi na Taarifa ya Kamati ya Ukaguzi.

Kwa upande wake, Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Mussa Budeba amempongeza Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi hiyo kwa maelekezo yao mazuri na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote uliotolewa na Bodi hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Budeba amesema GST imeandaa vipaumbele sita kwa lengo la kufanikisha mpango wa utekelezaji wa Vision 2030 ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa taarifa za kina za Jiofizikia kwa kurusha Ndege kutoka asilimia 16 ya sasa hadi asilimia 50 ifikapo Mwaka 2030.

Kikao hicho, kimehudhuriwa na Wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Jiosayansi Dkt. Dalaly Kafumu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi, Bertha Sambo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala CPA Constantine Mashoko pamoja na Menejimenti ya GST.

Share To:

Post A Comment: