Kampuni ya simu ya Halotel leo imezindua kampeni nyingine mpya kwa wateja wake inayokwenda kwa jina la Vuna Point.

Vuna point ni kampeni ambayo Halotel inaonyesha kujali na kuthamini wateja wake wajisikie wao ni wathamani hasa katika kupata huduma nzuri za mawasiliano.

Vuna point  ni kampeni ya wateja wanaoonyesha uaminifu wa kutumia mtandao wa Halotel kwa kupata bonasi ya pointi kila akionge muda wa maongezi kupitia vocha ya kukwangua au kwa Halopesa pia kwa kufanya miamala ya pesa na pia kwa kununua vifurushi kwa Halopesa.

Pointi hizi za bonasi zinaweza kuvunwa na kuwa dakika, SMS au MB.

“Mteja anaweza kuvuna pointi kwa kupitia MyHalo App au kwa kupiga *148*66# kisha chagua VUNA POINT. Pointi zilizovunwa zinaweza kubadilishwa na kuwa SMS, dakika, MB au namba ya Bahati itakayotumika kushiriki michezo ya Bahati nasibu ya Halotel.

“Akiongea Bw. Abdallah Salum ambaye ni Mkuu wa Sekta ya  Biashara  katika uzinduzi wa kampeni hiyo.

“Halotel itaendelea kutoa huduma bora kwa gharama nafuu huku tukiendelea  kuwa karibu na wateja wake kila siku, kwa kubuni na kuzindua michezo mbali mbali  kama sehemu ya kendeleza burudani na kufurahisha wateja wetu kwa kuchagua mtandao wetu wa Halotel katika huduma za mawasiliano nchini.

Share To:

Post A Comment: