Na Mwandishi wetu-Hanang'

Wanawake wa Baraza kuu la wanawake wa kiislam Tanzania mkoa Manyara ,wamefika katika mji wa Katesh wilayani Hanang mkoani humo, na kutoa mkono wa pole Kwa wawanawake wenzao wa kiislam waliondokewa na wenza wao katika mafuriko yaliyotokea Disemba 3 mwaka huu.

Akizungumza mwenyekiti wa baraza hilo wa mkoa manyara, Zainab Sige amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kusikia kuwa Kuna wanawake wa kiislam ambao wamefiwa na waumezao hivyo Kwa mujibu wa dini hiyo mwanamke anapofiwa na mume wake anapaswa kukaa Eda ,hivyo na wao Kwa Umoja wao Wanawake hao ndipo waliamua kijichangisha wao wenye na kununua mavazi mbalimbli na kwenda kuwavisha na kuwaweka Eda wanawake hao.

Moja ya wanawake waliopata msaada huo ni Khadija Said, ambaye amefiwa na mume wake na watoto wawili, ambapo  mwili wa mtoto mmoja hajaupata mpaka Sasa,amesema  wakati mafuriko hayo yanatokea yeye alikuwa safari na asubuhi ya tukio alimpigia simu mume wake Kwa ajili ya kumsalimia na watoto lakini simu hazikupatika,ndipo baadae alipigiwa simu na shemeji yake na kupewa taarifa za tukio hilo na kuwa mume wake na watoto wawili tayari wameshafariki na mtoto mmoja ameokolewa na yupo Hospitali.

Khadija amesema Kwasasa mtoto mmoja aliye Baki anaendelea vizuri na kuishukuru Serikali, mashirika na Taasisi mbalimbli pamoja na Baraza hilo la wanawake Kwa kufika kumuona na na kumfariji na  kuendelea kupokea misaada mbalimbli ikiwemo Chakula pamoja na mavazi.

Aidha Baraza kuu la wanawake wa kiislam Tanzania lilianzishwa mwaka 2002,na Kwa mkoa manyara limeanzishwa mwaka 2006 na kusajiliwa mwaka 2008,hivyo kufanya baraza hilo  lipo kiaheria.

Share To:

Post A Comment: