N

a John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amesema Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kupeleka maendeleo wilaya ya Babati katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Mheshimiwa Sillo amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan Jimbo la Babati Vijijini limepokea zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9  kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 98 kwa shule za Sekondari pekee.

"Kila mahali katika nchi hii kuna kazi zinafanyika, miundombinu ya barabara, maji, hospitali, ujenzi wa shule na kwa mara ya kwanza wazazi hawajaambiwa wachange kujenga shule na kununua madawati, katika historia ya nchi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili zaidi ya madarasa 20,000 yamejengwa," alisema Sillo.

Amezungumza hayo wakati wa maombi maalum ya pamoja ya  kumuombea, yaliyoandaliwa na Wanafunzi,Walimu, na Wazazi yaliyofanyika shule ya Sekondari Qash ikiwa kama zawadi kwao kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya.

Mkuu wa shule ya Sekondari Qash Mwalimu Ezekiel Kabogo amesema shuleni hapo Wanafunzi wanatoka umbali mrefu hivyo serikali iangalie namna ya kujenga mabweni
Amesema kinachopaswa kufanywa na kila mmoja ni kumuunga mkono Mbunge kwa kumpa moyo na kuthamini yale anayofanya Jimbo la Babati Vijijini.

Hata hivyo Sillo ameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo Ujenzi wa mabweni ili kuwapunguzia Wanafunzi mzigo wa kutembea umbali mrefu kwenda shule.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kata ya Qasha Idd Matata na Katibu wake Mohammed Issa wamesema wanafurahi kuona ilani inatekelezwa kwa vitendo na kwamba 2025 watamlipa wananchi wataamua zawadi watakayompatia Mbunge Daniel Sillo.

Aidha kwa fedha zake pekee kutoka kwenye mshahara wake ameendelea kutoa msaada wa kununua mashine za kutoa photocopy kusaidia kuchapisha mitihani shule za Sekondari.
Pia Mbunge alizungumza na wazee wa kata ya Galapo ambao nao walimfanyia maombi.
Share To:

Post A Comment: