Na  John Walter-Manyara

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na timu kutoka Wizara ya Afya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wametembelea eneo lililoathirika na maporomoko ya matope yaliyopelekea vifo vya watu 89 na majeruhi 139 Wilaya ya Hanang Mkoni Manyara.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy amebainisha mambo kadhaa yatakayoendelea kutekelezwa na Serikali ikiwemo kupeleka magari Matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance), kujenga kituo cha Afya katika eneo lililotengwa na Serikali kwa makazi ya watu.

Aidha Waziri Ummy Mwalimu ametembelea na kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Vituo vya Afya, Zahanati na kuzungumza na watumishi wa Afya pamoja kuwajulia hali majeruhi Watano (5) wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ambao ni waathirika wa maporomoko ya matope.

"Pia Serikali itaendelea kuwahudumia majeruhi waliobakia kwa sasa ambao ni Watano kwa gharama za Serikali Kama alivyoelekeza
Share To:

Post A Comment: