Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amempongeza Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kuwaunganisha wanawake na kuwawezesha kiuchumi ili waweze kuondokana na hali ya kuwa na utegemezi

Mwalunenge ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano mkuu maalum wa  UWT Mkoa wa Mbeya ulioandaliwa na Mhandisi Mahundi na kuahidi kuwaunga mkono katika uanzishwaji wa SACCOS ili kuwakwamua kiuchumi waondokane na mikopo ambayo imekuwa ikiwaumiza.

Aidha amewahimiza kushikamana wasihuri dini na ukabila ambayo yanawagawa Watanzania na kuagiza Wabunge wa Majimbo kuiga mpango huu ili kuwakwamua wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi Naibu waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mbeya amesema kuwa ubunge sio fashion na kuwa sio mtu anaamua tu kuwa mbunge utakuwa umefeli na kwamba ubunge ni uwakilishi lazima uwasababishie wenzio hao waone dhamani na faida ya kuwa na Mbunge na ifike mahali mtu akitaka kugombea ajipime .


"Sio sababu umemuona mtu fulani mmelingana kimo basi nawe unataka ugombee uwe na sababu ya kugombea ubunge na ujue unachoenda kufanya ,akina mama tukidhamilia tunaweza Sana hivyo tujitume kufanya shughuli mbali mbali za kujiongezea uchumi na kufanya makubwa ya kushangaza dunia kumbe umethamini 1000 yako na ukawa msaada kwa familia nzima "amesema.

Aidha Mhandisi Mahundi ameongeza kuwa kufanikiwa wanawake inawezekana kwani vyote vipo mikononi mwao na kusema kuwa wakate shauri na kudhamilia kikubwa kujenga nia ya pamoja.

Mhandisi Mahundi amewakutanisha wanawake wa wilaya Saba za mkoa wa mbeya lengo likiwa ni kuwawezesha kiuchumi zaidi kuwasisitiza na kushikamana ili kumpa kura za kishindo Mh.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwezesha uchaguzi wa serikali za mitaa.


Share To:

Post A Comment: