Na John Walter-Manyara

Sheikh wa mkoa wa Manyara (BAKWATA) Alhaj Sheikh Muhamad Khamis Kadidi  ametoa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maporomoko ya tope, mawe na Magogo wilayani Hanang'.

Misaada aliyoikabidhi Sheikh Kadidi ni Fedha taslimu shilingi Milioni 1,07,400, nguo, sabuni ya unga,taulo za kike, Mafuta ya kupaka, dawa za meno na miswaki.

Sheikh Kadidi amesema wataendelea kuiunga mkono serikali kila wanapojaliwa kupata chochote kutoka kwa Waislamu mkoani humo.

Akipokea misaada hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang' Francis Namaumbo amemshukuru Sheikh wa mkoa kwa msaada walioutoa akiwataka wengine waige moyo huo wa Upendo wa kusaidia waathiriwa wa Maafa hayo.

Share To:

Post A Comment: