Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa Waziri  Prof. Adolf Mkenda imekutana na kuwa na kikao cha pamoja Wadau wa Maendeleo wanaochangia katika Sekta ya Elimu nchini kutoka Balozi na Taasisi  mbalimbali za Kimataifa.

Katika kikao hicho wadau wamepongeza juhudi za Serikali katika  kuongeza uwekezaji katika elimu na kwa kusimamia vema  utekelezaji wa Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo na Mabadiliko ya Mitaala. 

Wadau hao kwa pamoja wameahidi kuendelea kuchangia maendeleo ya elimu ili kujenga nguvu kazi yenye ujuzi kwa maendeleo kupitia utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo.

Share To:

Post A Comment: