MKUU wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendinga,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy,akitoa hotuba ya ukaribisho wakati Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka,akizungumzia mikakati ya Wizara ya Nishati wakati wa Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu,akizungumza wakati wa Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendinga (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

MKUU wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendinga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

MKUU wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendinga,akiteta jambo na Viongozi mara baada ya kufungua Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

Na.Alex Sonna

MKUU wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendinga,ametoa wito kwa REA na Wabia wa Maendeleo kuweka Mikakati ambayo itawezesha maeneo yote nchini kufikiwa na huduma ya Nishati ya Umeme.

Mhe.Sendinga ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Mwaka Kati ya Wabia wa Maendeleo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara.

''Tunatamani tuione Tanzania yote inawaka. Ni matumaini yangu kuwa katika Mkutano huu mtajadili na kuweka mikakati na mipango itakayowezesha wananchi vijijini kufikiwa na huduma bora ya umeme''amesema RC Sendinga

Aidha ameipongeza REA kwa usimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy,amesema lengo la Mkutano huo ni kutathimini utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, amesema kuwa Wizara ya Nishati itahakikisha kuwa fedha za Wabia wa Maendeleo zinatumika ipasavyo kwa ajili ya kusambaza nishati vijijini na kuleta tija kiuchumi.

Awali Meneja Miradi Umoja wa Ulaya, Mhandisi Francis Songela amesema kuwa Miradi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa sana na wamejiridhisha baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi na kuona kasi ya utekelezaji ni nzuri.

''Tumeona faida ya miradi hii hasa katika kuleta mapinduzi kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi''amesema Mhandisi Songela

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: