"Utaratibu huu wakubadilishana uzoefu kati ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na Manispaa ya Temeke ukazae ushirikiano baina yetu".
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika katika kikao cha majumuisho ya ziara yakutembelea miradi iliyofanywa na Madiwa na wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema kubadilishana uzoefu kuwe kwa ustawi mzima wa maendeleo ya taasis hizo mbili ambayo itampa heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake,Naibu Meya wa Jiji la Arusha Abraham Mollel amesema mambo yote ambayo madiwani na wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha wamejifunza wataenda kuyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mhe.Mollel amesema, yale yote ambayo wamejifunza Madiwani na Wataalam wataenda kuyatekeleza kwakuwa ndio lengo kubwa ya ziara hiyo ya kikazi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa na wataalam wote, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Kamala Simba amesema mambo mazuri waliyojufunza yanaenda kuwa chachu kwa watendaji kwa kuhakikisha mipango yote iliyowekwa inatekelezwa kwa kiwango cha juu.
Pia, kuongeza umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya Madiwani na wataalam.
Katika kuhakikisha yote mazuri yanatendeka na miradi inakamilika kwa ubora Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema wao wanashikana mkono na kuwa kitu kimoja ndio maana wanaweza kutembea pamoja.
Ziara ya Madiwa na Wataalam kutoka Jiji la Arusha imefanyika kwa siku ya pili katika manispaa ya Temeke na miradi mbalimbali waliipitia kwa lengo la kujifunza kama vile; Ujenzi wa Soko la Zakhiem, Kituo cha afya Mbagala na ujenzi wa Barabara ya Kilomita 10 pamoja na Daraja la Kilungule.
Post A Comment: