Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde  ameahidi kuwatafutia fursa za kandarasi mafundi wa Dodoma kushiriki katika ujenzi wa Jiji la Dodoma unaonendelea kwa kasi hivi sasa.

Mavunde ameyasema hayo jana katika ukumbi wa Vijana wakati alivyokutana na kuzungumza na Mafundi zaidi ya 1000 wa Dodoma Jiji ambao walikuwa wameandaliwa mafunzo ya ufundi kutoka Kampuni ya Magic Builders International Ltd.

“Tunamshukuru sana Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa azma ya serikali yake ya kuiendeleza Dodoma na hivyo kuchochea maendeleo ya Jiji la Dodoma na kutengeneza fursa za Kiuchumi.

Nitahakikisha nawasimamia na kuongoza katika kuzifikia fursa hii kwakuwa ninyi lazima muwe sehemu ya uendelezaji wa Jiji la Dodoma.

Sheria ya manunuzi ya umma inataka Taasisi nunuzi kutenga 30%  ya manunuzi yake kwa ajili ya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu,hivyo nitahakikisha nasimamia kwa dhati ili kupitia umoja huu ninyi muwe wanufaika pia.

Ninataka tujenge umoja wa mafundi utakaozingatia uadilifu,uaminifu na uweledi.Kwa kuanzia nitawasaidia kupata ofisi na kuwalipia kodi kwa mwaka mmoja sambamba kuwapatia vitendea kazi vya ofisi”Alisema Mavunde

Akizungumza kwa niaba ya mafundi Dodoma Ndg. Twalib Ibrahim amewashukuru Mbunge Mavunde kwa kukubali kuwa Mlezi wao na pia kwa misaada mbalimbali ambayo amenuia kusaidia mafundi lakini Kampuni ya Magic Builders Int Ltd kwa mafunzo na kuwajengea uwezo mafundi wa Dodoma.

Share To:

Post A Comment: