MKURUGENZI wa Taasisi ya Agrithaman Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira, amesema taasisi hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuhifadhi,kuandaa na kuongeza thamani mboga na matunda

Akizungumza baada ya kukagua kiwanja ambacho kitatumika kutekeleza mradu huo, Neema, amesema mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho unathamani ya shilingi bilioni 2.4 na kitajengwa Bukoba Mjini mkoani Kagera.

Aidha, Mbunge huyo amesema, mradi huo upo chini ya ufadhili wa Mfuko wa Msaada wa Serikali ya Poland.

“Mradi wetu wa kiwanda cha Agrithaman cha kuhifadhi, kuandaa, kuongeza thaman mboga na matunda wenye thamani ya shilingi bilioni 2.4 utaanza rasmi baada ya kukabidhiwa kiwanja Bukoba Mjini.

“Mradi wa kiwanda hicho upo chini ya ufadhili wa Mfuko wa Msaada wa Serikali ya Poland, pia naushukuru uongozi wa mkoa wa Kagera kwa ushirikiano,”amesema


Share To:

Post A Comment: