Serikali wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha imesikia kilio cha wananchi wa eneo la Oldonyosambu kitongoji cha Masusu ambao kwa muda mrefu walikuwa wanatumia maji  yasio safi na salama ambayo walikuwa wanayatumia na wanyama ambapo serikali imekamilisha mradi wa maji uliogharimu zaidi ya bilioni 6.5 ambao umekwenda kuondoa adha iliyokuwa inawakabili.

Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi kwa kusimamiwa na Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini ambao umeondoa changamoto ya wananchi wa kata zaidi ya mbili ambazo walikuwa wakifuata maji umbali mrefu.

Joseph Johnson ni mkazi wa Kitongozi cha masusu ambapo ameishukuru Serikali kwa kufanikisha na kukamilisha ujenzi wa mradi huo na kuwaondolea adha familia zao zilizokuwa zinatumia muda mwingi kwenda kutafuta maji.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kututatulia changamoto ya maji kafika kata yetu, amesaidia wakina mama  na wanawake wetu ndoo kwa jitihada zake za kufanikisha mradi huu na miradi mingine,tunaomba Rais aendelee kutukumbuka wana Ngorongoro kwa kutuletea miradi ya maendeleo”

"Niwapongeza Sana ndugu zangu RUWASA kwa kazi kubwa na zuri wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi waishio vijiji wanapata maji Safi na salama, mwanzoni tulikuwa tunaona kwenye vijiji vya jirani ila kwa sasa wametufikia tuwashukuru sana" Alisema

Gerald Patrick Andrew ni meneja wa RUWASA wilaya ya Ngorongoro ambapo mewataka viongozi wa vyombo vya watumia maji (COWSOs)  kuhakikisha wailinda miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa wananchi.

“Boresheni huduma kwa wananchi vijijini ikiwa ni pamoja na kuwasongezea mtandao wa maji kwenye makazi yao sambamba na kutatua changamoto za kiufundi zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hii kukamiliaka,”amesema Gerald 

“Tulikuwa tunafuata maji kwenye mito ambayo nayo ikifika kipindi kama hichio cha mwezi wa nane inakauka tunaanza kutumia maji ya kwenye mabwawa kwa kweli hali ilikuwa mbaya lakini leo hii tunaishukuru Serikali imetuona na kuondoa tatizo la maji masusu” aliongezea

Mkazi mwingine wa kitongoji cha masusu Doreen Simon amesema kabla ya kupata huduma ya maji ndoa zao zilikuwa hatarini kwani walikuwa wanalazimika kuamka alfajiri Kwenda kufuata maji katika mabwawa ambayo yapo katika Kijiji cha Jirani hali iliyowalazimu kutumia muda mrefu kufuata maji.

“Kweli Rasi Samia Suluhu Hassan amemtua mama ndoo kichwani hapa kwetu masusu tulikuwa tunateseka tunatoka nyumbani alfajiri na watoto wale ambao ni wakubwa tumetumia maji ambayo usiku Wanyama nao walikuwa wanakunywa tunashukuru sana mwenyezi mungu anatulinda," Alisema

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala amesema kuwa ameagiza Ruwasa kuwasimamia wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya maji katika vijiji ili ikamilike kwa wakati na watakoshindwa atawachukulia hatua kali za kisheria.

“Ofisi yangu inataarifa za baadhi ya wakandarasi kuchelewesha miradi ya Maji,wapeni salamu hatutasita kusitisha mikataba yao sisi tunachotaka wananchi wapate maji kwa wakati kama mikataba yao inavyoelekeza,” Alisema Mangwala

Kwa upande wake Naibu Waziri wa maji Maryprisca Mahundi amesema fedha nyingi zimetumika katika mradi huo wa Masusu na kwamba kwa kuanza wamepata vichotea maji vichache lakini Serikali kupitia Wizara ya maji itahakikisha ukosefu wa maji unakuwa historia katika Wilaya hiyo.

"Sera ya maji inatutaka kutotembea umbali wa zaidi ya Kilometa 14 kutafuta maji na sisi tupo kuunga jitihada za Rais Samia kumtua Mama ndoo kichwani "Alisema

Amefafanua kuwa katika miradi hii inayotekelezwa na Serikali ya Rais Samia inapaswa itunzwe na wananchi na sio kuharibu miundombinu ya maji kwani itarudisha nyuma maendeleo ya upatikanaji wa maji.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alitembelea miradi ya maji katika kata ya Sale,enguserosambu,magaiduru pamoja na kijiji cha Wasso ambapo huduma ya maji kwa Wilaya ya Ngorongoro inatajwa kufikia zaidi ya asilimia 72.

Serikali imeendelea kutekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wote hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini ambapo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita imapata mafanikio.

(a) Serikali imeendelea kuimarisha huduma za maji Vijijini kwa kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu ya maji, hali iliyochangia upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Vijijini kuongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 67.7 mwaka 2015;

(b) Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma ya maji safi na salama Mijini. Kutokana na jitihada hizo, kiwango cha upatikanaji maji kwa wakazi wa Miji Mikuu ya Mikoa kimeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2005 hadi asilimia 86 mwaka 2014.

Aidha, katika jiji la Dar es Salaam pamoja na Miji ya Bagamoyo na Kibaha, kiwango cha upatikanaji maji kimeongezeka kutoka asilimia 55 hadi asilimia 68 katika kipindi hicho.

(c) Maabara za maji 16 na Kituo cha Utafiti cha kuondoa madini ya fluoride cha Ngurdoto kilichoko Arusha zimejengewa uwezo kwa kuzipatia dawa za kufanyia uchunguzi, mashine pamoja na usafiri.

 

Share To:

Post A Comment: