Na Imma Msumba ; Arusha
Rais Samia Hassan Suluhu anatarajia kufungua kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kitakachofanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9 ,mwaka huu Jijini Arusha
Akizungumza katika kikao cha Mawaziri cha Kujadili Maandalizi ya Kikao hicho Jijini Arusha Waziri wa Katiba na Sheria,Balozi Dk,Pindi Chana alisema maandalizi yanakwenda vizuri na wageni zaidi ya 700 kutoka mataifa mbalimbali watashiriki.
Balozi Chana alisema mbali na kujadili masuala ya msingi yanayohusi haki za binadamu na watu lakini pia watapata fursa ya kuitangaza nchi kwa mataifa mbalimbali juu ya utajiri na rasilimali zilizopo nchini.
Alisema kikao hicho kitabainisha mikakati mbalimbali ya mkutano huo kama fursa ya kiuchumi na kuimarisha taswira ya nchi katika masuala ya haki za binadamu na watu.
Pia taarifa ya hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kikao cha 77 cha kawaida cha kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu sambamba na kushauri namna bora ya kufanikisha kikao hicho
"Serikali itatoa ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekaji wa mazingira wezeshi katika kufanikisha mkutano huu"
Alisema masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo maadhinisho ya siku ya haki za binadamu kwakuzingatia itifaki ya Maputo,taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu Barani Afrika,uzinduzi wa nyaraka mbalimbali za kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,taarifa ya wanaharakati wa haki za binadamu na wau,kuidhinishwa kwa itifaki ya mkataba wa Afrika wa Ulinzi wa Jamii.
Lakini pia uwezeshaji wa wanawake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hali ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi Barani Afriak na Msaada wa Kisheria na Upatikani wa Haki
Kwamujibu wa Balozi Chana alisema mkutano huo unahisisha sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya kimataifa,utamaduni,sanaa na michezo,fedha na uchumi,ulinzi na usalama ,afya ,habari na mawasiliano.
Post A Comment: