Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa niaba ya Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso Jumaa aweso ameitikia wito wa kushiriki kwenye majumuisho ya ziara ya

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Katavi wakati wa majumuisho wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM

Nougu Daniel Godfrey Chongolo, Mhe Mahundi amesema kuwa katika kuboresha huduma ya maji katika mji wa Mpanda, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 ambapo mpaka sasa Mkandarasi anaendelea na kazi. 

Aidha, kwa miradi ya Mamba- Majimoto a Kapalamsenga - Karema Serikali tutaendelea kusimamia na kufuatilia ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati "amesema"

Ameongeza kuwa katika mpango wa muda mrefu Serikali itatumia chanzo cha Ziwa Tanganyika ambapo taratibu za kumpata mtaalam Mshauri zinaendelea na ataanza kazi Mwezi Desemba, 2023

Pia, Mheshimiwa Mahundi amemuahaidi Katibu Mkuu wa CCM kuwa atafika kwenye mradi wa maji wa Ugalla uliopo Wilayani Nsimbo kufuatilia Utekelezaji wake na kuweze kutoa maelekezo kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

Share To:

Post A Comment: