Tanzania imetajwa kuwa kinara katika nchi za Bara la Afrika katika utekelezaji wa mpango wa Anwani za makazi ambapo mitaa yote imeweza kutambuliwa na kupewa majina kwa asilimia 95.  

Hayo yameelezwa na Mhandis Jampyon Mbugu  ambaye ni Mratibu wa mfumo wa  anwani za makazi kitaifa kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia 
akiwa mkoani Morogoro.  

Kutokana na kuwepo kwa ufanisi katika utekelezaji wa mpango huo Tanzania  sasa inajivunia kushika nafasi ya kwanza  kwa nchi za bara la Afrika ambapo kwa sasa mitaa yote imeweza kutambuliwa.

Katika kuhakikisha Mfumo huo unakuwa endelevu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia  ya habari inawakusanya wenyeviti wa mitaa,watendaji wa mitaa ,watendaji wa kata  na  wakusanya taarifa ili kuwapa mafunzo ya namna kuweza kuhakiki taarifa za anwani za makazi katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro.
MWISHO. 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: