Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( wa tatu kushoto) akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma  Arusha,Husin Sjat baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za  Puma Energy Tanzania mwaka 2023.Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Puma Dk.Seleman Majige na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma nchini Tanzania Fatma Abdallah.

 PUMA Energy Tanzania imeendeleza utaratibu wa kuwatambua watoa huduma bora kwa mwaka 2023 ambapo imetoa tuzo na fedha kwa washindi ambao wanatoka maeneo mbalimbali nchini ambako Puma inatoa huduma zake kwa Watanzania kupitia biashara ga mafuta, gesi na vilainishi.


Pamoja na kutoa tuzo hizo kwa watoa huduma wake katika vituo vya mafuta vya Puma, pia imeahidi kuendelea kusimama imara kuendeleza rekodi ya kuwa kampuni namba moja ya mafuta nchini huku ikisisitiza ubora wa bidhaa zake.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwatangaza na kuwapa zawadi waendeshaji bora wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Fatma Abdallah amesema mafanikio makubwa inayoyapata kampuni hiyo na kuendelea kuwa namba moja katika soko yanatokana weledi, kujituma na uwajibikaji unaofanyika vituoni.

Amesema watoa huduma hao wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma iliyobora kila wanapotembela vituoni, hivyo watoa huduma hao ndilo jicho la kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Fatma lengo la Puma Energy Tanzania ni kuendelea kutoa huduma bora Watanzania zinazohusu mafuta, gesi na vilainishi na mkakati wao ni kuendelea kuboresha huduma kulingana na wakati na mahitaji hasa ya kuongeza vituo vya mafuta.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, mbali ya kuwapongeza Puma katika kutoa huduma katika sekta hiyo pia amesisitiza Serikali imeridhishwa na mwenendo wa kampuni hiyo katika utoajia wa huduma za mafuta, gesi na vilainishi na kuahidi kuendelea kuwa nayo bega kwa bega.

Pia ameipongeza kwa ubunifu unaofanywa na kampuni hiyo ukiwemo wa kuwatambua watoa huduma wake na kuwapa tuzo kama ishara ya kutambua ba kuthamini mchango wao katika utoaji huduma bora.

Amesisitiza kwamba huduma bora ndizo zinazoifanya kampuni hiyo iendelee kuwa namba moja kwa utoaji wa huduma za mafuta nchini, hivyo itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inaendelea kuwa katika ubora unaitakiwa na kuiletea nchi mapato zaidi.

Amefafanua taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Puma Energy Tanzani ni kiongozi wa soko katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli nchini.


Share To:

Post A Comment: