Na Ashrack Miraji, Same kilimanjaro.

Mbunge wa Same Mashariki Mhe.Anne Kilango Malecela ameiomba Serikali kuwaongezea fedha wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Same ili waweze kujenga daraja la kuunganisha Kata ya Kirangare na Mpinji.

Akizungumza na wananchi wa  Kata Kirangare wakati akitambulisha Mradi wa Ujenzi wa Barabara  ya Idaruu-Narema yenye urefu wa kilomita 7 Mheshimiwa Kilango alisema Ujenzi wa Barabara hiyo ni muhimu sana kwani utasaidia kuunganisha wananchi wa Kata ya Kirangare na masoko.

Amesema bado wananchi wa Kirangare ambao wanategemea soko la Myamba hawataweza kuvuka upande wa pili hadi daraja hilo litakapokuwa limejengwa

Hivyo nitakuwa mchoyo wa fadhira kumshukur Dakt Samia Suluhu Hassani kuendelea kuwadhamin wananchi wake kwa ujenzi wa barabara hiyo ambao utaghalimu million 395 kwenda kumaliza kero kwa Wananchi pia na kumpongeza ndugu yang Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni anaifanya Kazi kubwa Sana hasa Katika kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo Katika wilaya hii amesema Anna kilango mbunge wa.  Same Mashariki

Akizungumza katika hadhara hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameahidi kuwasilisha maombi hayo ya kujengewa daraja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dakt Samia Suluhu Hassan ili aweze kuwasaidia wananchi hao.  

Serikali ya Awamu ya sita ambayo inaongozwa na jemedali wetu Dakt Samia Suluhu Hassani ni Serikali sikivu na inajali maslahi ya wananchi wake hivyo ntapambana kwa juhudi zangu zote Hili ujenzi huo uweze kukamilika na kuondoa kero kubwa kwa Wananchi wa kirangare na mpinji alisema Kaslida Mgeni

Kwa Upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Same Mhandisi James Mnene amesema barabara hiyo ya km 7 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe inagharimu jumla ya shilingi milioni 395 ambazo no fedha za tozo.

Kuhusu Ujenzi wa daraja la kuunganisha Kata hizo mbili Mhandisi Mnene amesema TARURA itakokotoa gharama za Ujenzi na kuwasilisha TARURA Mkoa kwaajili ya kuomba fedha za Ujenzi maana lina umuhimu mkubwa. 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: