NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amezionya kampuni za uuzaji wa mafuta dhidi ya kuhodhi mafuta, kitendo ambacho kinasababisha uhaba na kusababisha ongezeko la bei.

“Hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria,” Kapinga alisisitiza mwishoni mwa juma aliposhinda tuzo ya mfanyabiashara wa Puma Energy Tanzania iliyofanyika jijini ar es Salaam.
Hafla hiyo mwaka huu imelenga katika kutambua mchango wa wafanyabiashara wa Puma Energy katika hafla hiyo, Naibu Waziri ameitaka Kampuni ya Puma Energy Tanzania kupeleka maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa mafuta umekuwa changamoto.

Amesema mapaka sasa, kampuni hiyo ina vituo 74 vya mafuta, lakini idadi hiyo bado ni ndogo kwa kuzingatia ukubwa wa kampuni na changamoto za usambazaji wa mafuta hususani maeneo ya vijijini.

Akizungumzia tuzo hiyo, Kapinga ameiomba kampuni hiyo kuifanya iwe endelevu na kuhakikisha inawekeza kwa kiwango kikubwa katika Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), hususan katika elimu ili kusaidia nchi kuzalisha wataalam zaidi wa sekta ya mafuta na gesi.

Awali, akimkaribisha Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma, Selemani Majige, alimshukuru Rais, Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake, na kuahidi kuwa kampuni hiyo itahakikisha upatikanaji wa mafuta zaiidi, aidha kujenga vituo vingi vya mafuta hususani maeneo ya vijijini.
Share To:

Post A Comment: