.

 Na Janeth Raphael Dodoma


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amekabidhi Ofisi kwa mrithi wake Mobhare Matinyi huku akieleza kuwa anaondoka akiwa na jambo linalomsumbua la hali ya vyombo vya habari na uchumi wa waandishi wa habari.

Msigwa ameyasema hayo leo Oktoba 6,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Idara ya Habari Maelezo kwa Matinyi ambaye kabla ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Msigwa ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema " jambo ambalo nilitamani kulifanyia kazi ni kuhakikisha uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari unaimarika na nimeondoka wakati bado haujaimarika na kupelekea waandishi wengi kufanya kazi hiyo kwa kujitolea badala ya kupata ajira zinazoweza kuwapatia kipato,"

Kwa upande mwingine Msigwa ameahidi kutekeleza wajibu aliotumwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhakikisha Wizara hiyo inaleta furaha kwa watanzani kiuchumi na kiafya.

Amewashukuru waandishi wa Habari na kutaka ushirikiano huo uendelee kwa msemaji mpya huyo aliye

Kwa upande wake Mkurugenzi wa habari maelezo Mobhare Matinyi ameahidi kufanya kazi kwa juhudi zote kwa kushirikiana na Taasisi zote ili kutimiza malengo ya Mhe. Rais za kutangaza kazi zinazofanyika

Matinyi ameahidi kushirikiana na Waandishi wa Habari kwa kuhabarisha umma juu ya Mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita.

Pia emeongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kutumia vyema kalamu zao kwenda kwa wananchi kuandika mazuri yanayofanywa na Rais Samia katika kuwaleta maendeleoShare To:

Post A Comment: