WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) umeungana na vijana zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali duniani kupanda miti ya mikoko 1000 katika maeneo ya Kunduchi na Mbweni jijini Dar es Salaam.
Lengo la TFS kuungana na vijana hao ni kuendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameendelea kuleta athari duniani kote.
Vijana walioshiriki upandaji miti ya mikoko wanatoka katika mataifa 24 na wapo nchini kwa ajili kushiriki Kongamano la tatu la Kimataifa la Viongozi Vijana na Mabadiliko ya tabianchi (GLOBAL YOUTH CLIMATE SUMMIT) linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Oktoba 6, 2023 wakati wa upandaji mikoko Naibu Kamishina wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Zainab Bungwa aliyemwakilisha Kamishina wa Uhifadhi wa Wakala huo Profesa Dos Santos Silayo amesema vijana hao wameongozana na Ejaj Ahmad ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Uongozi wa Vijana na Mabadiliko ya Tabianchiwa Kimataifa Ejaj Ahmad
"TFS tumeona sasa kupitia kituo hiki tuungane na watanzania wenzetu na hasa vijana katika kupanda mikoko lakini kuweka mikakati ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
"TFS tuko chini ya Wizara ya Maliasili na utalii na maono yetu ni kuhakikisha tunasamia misitu na nyuki lakini tunakuwa ni kitivo cha taifa.Pia tunasimamia , tunaendeleza kwa ajili kizazi cha sasa na cha baadae...
"Na ndio maana leo hii tumepanda mikoko ambayo ni muhimu sana katika ulinzi wa pwani na sio pwani tu lakini kidunia na katika upande hewa ukaa mikoko inaweza kunyonya tani nne mpaka tani 10 zaidi ya misitu mingine
"Kwa hiyo misitu ya mikoko ni muhimu sana kwa uhifadhi lakini ni muhimu kwa ajili ya kukabidili mabadiliko ya tabianchi ambayo yameikumbuka dunia na Tanzania ikiwemo, " amesema Bungwa.
Amefafanua mabadiliko ya tabianchi yameendelea kusababisha mafuriko na ukame kwani mvua hazinyeshi huku akifafanua TFS imeendelea kuhamasisha wanapanda aina mbalimbali ya miti na vijana wawe mstari wa mbele kuitunza.
Ametumia nafasi hiyo kuileza dunia kuwa kama mikoko hiyo wataitunza wataweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi lakini kama vijana wakielewa n kuhamasishwa watakuwa kundi muhimu katika kutunza misitu.
Pamoja na hayo ametoa rai kwa wawekezaji kuwekeza katika maeneo ya utalii wa misitu na kuhusu mikakati yao ni pamoja na kujenga uelewa wa vijana wa Tanzania nzima lakini pia kuwapatia utalaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Uongozi wa Vijana na Mabadiliko ya Tabianchiwa Kimataifa Ejaj Ahmad amesema amefufahi kuona vijana hao wameshiriki upandaji miti ya mikoko.
"Miti ya mikoko inafaida nyingi ikiwemo ulinzi katika maeneo ya pwani lakini inasaidia kunyonya hewa ukaa , hivyo uwepo wa mikoko unaokoa maisha yetu.Mbali na upandaji mikoko vijana hawa wamepata nafasi ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi."
Awali Mwanaharakati wa mazingira na Mwanasayansi ya Jamii Shamimu Nyanda amesema ni muhimu vijana kushiriki katika uhifadhi na utunzaji mazingira sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Post A Comment: