Na Tumaini Mafie,ARUSHA


Rais wa Asasi za Kiraia nchini Stigmata Tenga Amesema wataboresha Mahusiano na Asasi zisizo za kiserikali Kwa sababu sauti wanazozipeleka ni za wananchi hivyo  wanahitaji kupeleka tenda nyingi kwa ajili ya kuhudumia watu wake huku akidai wanashindwa kupokea tenda hizo Kwa dhana ya kufananishwa na Asasi zisizozakiserikali.

Amesema katika kuboresha mahusiano kwenye sekta wanatoa mapendekezo ya kuomba kusogeza matamasha badala ya kufanya matamasha Ifikapo Octoba wafanye  Agost Kwa ajili ya kuwezesha ushiriki wa wananchama wengi Kwa kuwa yamekuwa yakifanyika karibu karibu hivyo kushindwa kutofautisha  Asasi za Kiraia na Asasi zisizozakiserikali.

"Watu wanashindwa kutofautisha Matamasha haya kutokana na kufanyika karibu karibu na pia wengine wanashindwa kuhudhuria makongamano haya, hakuna uwezo huo wa kusafiri mara mbili mara tatu Kwa ajili ya kuhudhuria haya matamasha hivyo tumeomba kusogeza Hadi Agost tar 26 Hadi 30 mwakani badala ya Octoba" Amesema  Stigmata.

Naye Mkurugenzi wa AZAKI Frances Kiwanga amesema anaamini ni wiki itakayoleta mabadiliko Kwa washiriki wote wa Asasi za Kiraia ambapo alishukuru Serikali Kwa Ushirikiano mzuri kati yao na Asasi hizo.

"Ni matumaini yangu kuwa Wiki hii imeleta mabadiliko Kwa washiriki ,nitoe wito kwa vijana kuleta mapinduzi makubwa kupitia teknolojia hususani tukizingatia namna ambavyo hapa tumekuwa tukijifunza kupitia waliofanikiwa kutumia hizi teknolojia" amesema Kiwanga.

Hata hivyo Kongamano la Asasi za Kiraia hufanyika Kila mwaka Ifikapo Octoba ambapo Kwa Sasa wametoa mapendekezo kufanyika Kila Agosti Kwa lengo la kushirikisha wadau wengi zaidi.

Share To:

Post A Comment: