Kamati ya Utekelezaji UVCCM-Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti Wake ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC) imetembelea na kukagua maboresho ya Bandari ya Mkoani na Kituo cha maegesho ya makontena ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2023.

Maboresho ya Bandari hio yamegharimu fedha kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo ni fedha za ndani, hii ni dhamira ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe. Dkt Hussen Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuhakikisha wananchi wanaweza kusafirisha bidhaa zao kwenda nje ya nchi lakini pia kuingiza bidhaa kutoka nje kuja Visiwani Pemba.

Ndugu Kawaida ameusihi uongozi wa Bandari hio kuhakikisha wanufaika namba moja wa ajira katika bandari hiyo ni vijana kitanzania hususani Vijana wa Pemba ambao wapo karibu na mradi huo.

Mwisho Ndugu Kawaida amewasihi wananchi wa Pemba kuitumia fursa ya bandari hiyo kwani ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi katika eneo hilo lakini pia itasaidia kupunguza mfumuko wa bei.

Lengo la ziara hii ni kuimarisha Uhai wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana, Kusikiliza hoja na Changamoto za Wananchi na kuzitatua, pamoja na  kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya CCM Mikoa ya Pemba ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020 - 2025 pamoja na miradi ya Chama na Jumuiya zake.








Share To:

Post A Comment: