Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Maji amefungua Mkutano wa mwaka wa Kimataifa wa Mtandao wa Wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Jiji Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan 

Wakati wa Hafla hiyo, Mhe. Mahundi amesema kuwa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, yapo zaidi ya Ishirini na moja (21) ambayo husababishwa na vimelea mbalimbali ikiwa ni pamoja na Minyoo, Bakteria, Virusi, na fangasi

Ameongeza kuwa katika nchi mbalimbali duniani, Tanzania ni miongoni mwa Nchi zikizoathirika na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambayo  ni Usubi, Trakoma, Matende na Mabusha ambapo takwimu zinaonesha kwamba takribani watanzania milioni 56 wapo katika hatari ya kuambukizwa angalau ugonjwa mmoja au zaidi kati ya haya.

Katika hafla hiyo, Viongozi mbalimbali wameweza kushiriki akiwemo Mheshimiwa John Samwel Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu

Share To:

Post A Comment: