Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa ameeleza kuwa kero ya maji sasa katika baadhi ya Kata za monduli imemalizika baada ya pampu ilikuwa imeharibika kufungwa mpya na itakwenda kuwasaidia wananchi hao baada ya kusota kwa muda mrefu.

"Kuna changamoto kubwa ya maji , na Kuna vijiji tangu nchi ipate uhuru havijawahi kuona maji ya bomba na nawaomba Tanesco ituachie angalau umeme kwa wiki moja wananchi hawa waweze kunufaika" Alisema

"Wizara ya maji ipo kwenye mpango wakuja kufanya makubaliano ya mkataba na wakandarasi kwa ajili ya kusambaza maji kwenye zaidi ya vijini 12 niwaombe wananchi wa monduli kuendelea kuwa watulivu muda sio mrefu serikali inakwenda kutatua kero hii ya maji kabisa kwenye Jimbo letu hili" Aliongezea 

Aidha Lowasa Kwa niaba ya wananchi wa Monduli ametoa shukrani nyingi na kuendelea kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea adha kubwa wananchi wake iliyowasumbua kwa zaidi ya miezi mitatu na hivi sasa Serikali imewafungia pump mpya ya kusukuma maji kutokea Ngaramtoni, ambayo tayari imeanza kufanya kazi ramsi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Joshua Nassari wakati akishuhudia ufungajiwa pampu hiyo amesema mradi huo wa maji ulikuwepo tangu miaka 20 iliyopita wakati wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa ambapo alipovuta maji hayo kwa zaidi ya kilomita 40 kutoka eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru.

Akizungumza kwa niaba ya Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Issack Joseph Copriano amesema tatizo sio pampu kufungwa ila cha muhimu ni wananchi kupata Maji , ambapo amemuomba Mkurugenzi wa AUWSA Mkoa wa Arusha kuhakikisha maji yanatoka wasije kufika Wilayani na kukuta hali ni ileile. 

Viongozi hao wamesisitiza wananchi pamoja na wadau wote wa maji kutunza miundo mbinu yote ya maji ili kuondokana na kero kubwa ya maji inayo athiri wananchi wa monduli.Share To:

Post A Comment: