Na; Elizabeth Paulo, Dodoma

Wakulima nchini washauriwa kulima kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati.


Hayo yameelezwa na Ndg.Ramadhani Mrutu ambaye ni Afisa mauzo kutoka kampuni ya Reliance Group ambao ni wauzaji na wasambazaji wa matrekta,vipuri na viunganishi vya matrekta aina ya sonalika.


Aidha amesema kuwa kampuni yao imejidhatiti kutoa huduma nzuri yenye kuaminika wakati wote na wanamatreka kuanzia madogo kabisa mpaka makubwa na wanatoa fursa kwa wakulima wadogowadogo kuweza kununua bidhaa hizo kwa gharama nafuu zaidi kwa kuwakopesha wakulima kwani wameingia ubia na taasisi mbalimbali za kifedha ambazo ni takribani 8 ili kuhakikisha wakulima wanaendana na kasi ya kilimo cha kisasa.



"Ningependa kuwashauri wanachi kununua bidhaa zetu ili kutoka kwenye kilimo cha mikono kwa kutumia jembe hadi kilimo cha kisasa kwa kutumia trekta ili kuendana na kasi ya sekta ya kilimo kwa kuokoa muda na kuendana na kasi ya uchumi wa kati"Amesema Ndg.Ramadhani


Aidha ameongeza kuwa kwa upande wa vikundi na mashirika huwa wanatoa elimu ni namna gani wakulima wanaweza kupata faida kupitia kilimo cha trekta ambapo mpka sasa bidhaa zao zimeshasambaa mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kati inayopatikana kibaigwa,kongwa na kanda za juu kusini mbeya,sumbawanga, kaskazini babati,mashariki ifakara morogoro,kanda ya ziwa kahama,Songea ambapo kusini inafika mpaka mtwara,kahama bariadi ili kuhakikisha wanamfikia kila mtanzania.


Aidha amesema kuwa trekta zao ni kuajili ya mkulima mdogo wa heka 20 hadi mkulima wa heka kubwa kuanzia heka 500,1000 na kuendelea hivyo wanamgusa mkulima kuanzia kuandaa shamba hadi mwisho.


Mtaalamu huyo ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanalima kilimo cha kisasa na chenye tija ili kuendana na kasi ya dunia kwenye sekta ya kilimo kwani kilimo ni uti wa mgongo hivyo walime kilimo biashara ikiwa ni ajenda ya nchi kulisha afrika na dunia kupitia sekta ya kilimo.


Trekta ya sonalika ni imara kutoka India zinazotengenezwa na kiwanda cha International Tractors Limited ambacho ndiyo kiwanda kikubwa kuliko viwanda vingine vyote vya matrekta India na kwa hapa Tanzania zipo sokoni kwa zaidi ya miaka 15 sasa,ni trekta zinazopatikana katika ukubwa tofauti na zinaweza kuhimili kila aina ya udongo na zinafaa kwa kilimo cha kila zao linalolimwa Tanzania.

 

Kauli mbiu ya maonyesho haya ya wakulima 88 ni "vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula"

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: