Na;Elizabeth Paulo, Dodoma 


Ili Sekta ya Kilimo ichangie ipasavyo katika vita dhidi ya umaskini serikali imelenga kukuza sekta ya Kilimo kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.


Kufikia lengo hilo Viajana na Wanawake ambao ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa lazima washiriki kikamilifu kwenye shughili za kilomo kwa kuzingatia uzalishaji wenye tija.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Balozi Pindi Chana amesema hayo Leo Agost, 4 alipokua mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kongamano la zao la Mtama katika maonyesho ya 15 sherehe za nanenane kanda ya kati yanayojumuisha Mikoa ya Singida na Dodoma yakifanyika viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.


“Serikali imepanga kubadilisha Kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa Kilimo cha kibiashara, Mabadiliko haya yanafanyika kwa kuzingatia malengo ya kitaifa kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya maendeleo 2025.”Amesema Balozi Chana.


Kumekuwa na mazao mapya na mageni ambayo yanalimwa katika Mikoa hii na hii inatokana na ukweli kwamba shughili za Kilimo ni huru na huria.


Hata hivyo ufanisi wa mazao haya umekua mdogo na usio wa uhakika katika kila msimu na katika kila eneo la Mkoa huu ukilinganishwa na wa mazao ya asili likiwemo zao la Mtama.

 

Waziri huyo amesema Mikoa ya kanda ya kati kama ilivyo kwa nchi na Dunia nzima inakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo haijatoa mwelekeo wowote wa kama Hali ya hewa imebadilika kuelekea wapi zaidi ya kutokua na uhakika wa hali ya hewa katika msimu huu na misimu mingine itakayofuata.


“Ni wa msingi huo Mikoa ya Dodoma na Singida imeamua kwa dhati kuendeleza zao la Mtama ambalo limekua likistawi vizuri kwa hali ya hewa ya Mikoa hii. ”Amesema Balozi Chana


Aidha amesema Mikoa ya Dodoma na Singida ni maarufu kwa Kilimo cha zao la Mtama wa aina mbalimbali huku umaarufu huo ukichangiwa na hali ya hewa inayopatikana maeneo mengi ya Mikoa hii kustawisha Vizuri zao la Mtama.


Kwa Muktadha huo huo, Mtama ni zao linalohimizwa kuzalishwa kwa ajili ya uhakika wa usalama wa chakula na kipato kufuatia Kuongezeka kwa uhitaji wa zao hilo hapa nchini na nchi Jirani kama Burundi, Rwanda, Southern Sudan na Kenya.

“Pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanyika, bado tija ya uzalishaji wa zao hili ni ndogo kutokana na Wakulima kutokutumia kanuni bora za Kilimo.”Amefafanua Balozi huyo


Balozi Chana amesema Mikakati mbalimbali ya kuleta mageuzi ya sekta ya Kilimo nchini inatekelezwa kupitia programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) ambayo inalenga kuleta mageuzi katika sekta ya Kilimo(Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu).

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: