Wananchi wakipewa elimu katika banda la TPHPA wakati walipotembelea maonesho Kimataifa ya Kilimo  Nane Nane , kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka TPHPA Profesa Joseph Ndunguru akiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane kwenye viwanja vya John Mwakangale , jijini Mbeya

MAMLAKA ya Afya ya mimea na Uthibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA),imesema katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane),imejipanga kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu ,vinyunyizi,udhibiti wa visumbufu vya Mimea,taratibu za uingizaji wa mazao nchini na utoaji wa mazao nje ya nchi pamoja na usimamizi wa biashara ya viuatilifu (taratibu za usajili wa Viuatilifu na biashara za viatulifu.


Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula', ambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoni hapa kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Akizungumza Jijini Mbeya leo Agosti 2,2023katika banda la Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka hiyo Profesa Joseph Ndunguru amesema uwepo wao katika maonesho hayo lengo kuu ni kutoa elimu kwa wananchi wa mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Mamlaka hiyo inatoa elimu juu ya uhifadhi wa bioanuai za mimea, udhibiti wa visumbufu vya mimea kwa kutumia njia za kibaolojia, na udhibiti wa wa visumbufu vya mlipuko.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya maonesho ya hayo 2023 kwa upande wa Mamlaka hiyo Dkt Mujuni kabululu amewaomba wananchi kuendelea kutembelea banda hilo ambapo watapata fursa ya kukutana na wataalumu ambao watajibu maswali yote na kutoa elimu stahiki pamoja na kupokea changamoto mbali mbali za wakulima
Share To:

Post A Comment: