Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini kupitia Mfuko wa jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma amekabidhi madawati 722 kwa halmashauri ya Kasulu Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini kwa mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Akikabidhi madawati hayo Mbunge wa jimbo hilo Prof.Joyce Ndalichako amefafanua kuwa madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 59 ambayo yatasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia ambapo amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha njia katika sekta ya Elimu.
Prof. Ndalichako amewasisitiza walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo ikiwa ni pamoja na kuonyesha nidhamu nzuri shuleni pia amesisitiza kuendelea kutumia fedha ya jimbo kwa maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali.Isaac Anthony Mwakisu amemshukuru mbunge huyo kwa msaada huo wa madawati na kueleza kuwa uwepo wake kwenye jimbo hilo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo na kuifanya wilaya hiyo kupiga hatua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kasulu Mji Bw.Noel Hanura ambaye ni diwani wa kata ya heru juu amemshukuru Prof. Ndalichako kwa kuwa mbunge Kiongozi ambaye pamoja na majukumu makubwa ya serikali aliyonayo amekuwa na utamaduni mzuri wa kukutana na wananchi na kutatua kero zao.
Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Dollar Kusenge amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya Madawati ambapo hapo awali halmashauri ilikuwa na upungufu wa madawati, 22,500 na pia ameendelea kumshukutu Rais samia kwani ameboresha mazingira latika nyanja za elimu,afya na mazingira kwa kuleta watumishi wa kutosha.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari bogwe bw.David Kindanda kwa niaba ya walimu wakuu wote amesema ,"Naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji na kwamba madawati waliyopewa leo yatasaidia kupandisha kiwango cha taaluma na kupunguza utoro".
Post A Comment: