Julieth Ngarabali. Kibaha 

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi Taifa ( NEC) Mkoani  Pwani  Hamoud  Jumaa amewataka wanachama na Viongozi wa CCM Kibaha Mjini kujenga mahusiano mzuri baina  yao ili kuweza kuwa na mshikamano na umoja

Jumaa amesema utaratibu huo ni silaha mojawapo kubwa ya kuweza kufanikisha ushindi kwa CCM katika uchaguzi ujao wa 2024 wa Serikali za mitaa ambapo pia itakua njia salama ya kufanya vizuri pia katika uchaguzi mkuu ujao.

Amesema hayo  kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka kata 14 akiwemo Mbunge  jimbo hilo Silvestry Koka,,mjumbe kamati ya siasa Alhaji Musa Mounsour pamoja na  Katibu siasa na uenezi Pwani  David Mramba.

Kuhusu michango au kusaidia chama Jumaa  amesema CCM haiwezi kujengwa na mtu mmoja hata siku moja na ndio maana katika fomu ya kugombea Ubunge, udiwani unagombea nafasi yeyote ile lazima utaulizwa chama hiki utakichangia nini ,kwa hiyo watoe misaada  kwa kufuata taratibu .

Pia amesisitiza  ni lazima Mbunge apewe nafasi ya kufanya shughuli zake kipindi cha miaka mitano akimaliza miaka yake mitano shughuli zingine zinaendelea 

"Mwenyezi Mungu anasema katika vitabu vyake  jambo ambapo mwenyezi mungu analitaka hakuna mwanadamu analipiga ukiandikiwa wewe kuwa katika nafasi fulan utakua tu hata Dunia nzima ikipinga"amesema Jumaa

Awali Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mwajuma Nyamka amewaeleza  wanachama kuwa Kibaha Mjini ipo salama na shwarii kisiasa ndani ya chama kuanzia kwenye matawii .

"Sitakua rafiki kwa mwanachama yeyote atakayetaka kuiviruga Kibaha Mjini kwa kisingizio cha kutoa misaada kwenye chama maana CCM haiwez kujengwa na mtu mmoja, bali na wadau mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali ili mradi tu afate taratibu"amesema Nyamka

Katika hatua ingine Mbunge wa eneo hilo Silvestry Koka amewashukuru  wana CCM na  Wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano katika kuijenga Kibaha na kuahidi ataendelea kukamilisha ahadi alizotoa ikiwemo ya ujenzi wa miradi mbalimbali na Ofisi za chama.

Naye Katibu wa siasa na uenezi wa CCM  Pwani David Mramba ametumia hadhara hiyo kuwaomba wanachama kuachana na mmomonyoko wakati huu ambapo chama kinaelekea kwenye uchaguzi mwaka 2024 na badala yake wasimame kwenye makusudi ya chama chao ili itakapofika 2024 kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wawe kitu kimoja.

'naombeni na ninawasihi sana , nasema haya kwa sababu ninaona na ninyi ni ndugu zangu na rafiki zangu tunaona kwenye mitandao namna ambavyo watu wanazungumza na hata lugha zao hazileti maana kwenye jamii yetu,naomba sana tusiwe wachochezi kwenye mitandao tusimamie misingi ya chama chetu ili siku moja tuje tupate ushindi wa kishindo 2024/2025 'amesema Mramba

Share To:

Post A Comment: