Na John Walter -Babati

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amekerwa na baadhi ya watendaji kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati, hali inayowalazimu kuwasubiri au kuwafuata viongozi wa ngazi za juu.

Kufuatia hali hiyo, Sendiga amewataka viongozi wote mkoani humo kujiwekea utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi na baada ya hapo apate ripoti ya hali ya migogoro na utatuzi wake kabla hazijamfikia.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Gedawari Wilaya ya Babati na kusikiliza kero zao Agosti 17,2023, amewahimiza watendaji wa kata, vijiji, maofisa tarafa, wenyeviti wa Mitaa na Vijiji,kutatua kero za wananchi kwa kuwafuata na sio kuwasubiri kwenye ofisi zao.

 Amesema kazi ya Kiongozi ni kuwahudumia Wananchi na  kushindwa kufanya hivyo kunawalazimu Wananchi kuzishughukikia wenyewe bila ufumbuzi na kukwama kufanya Shughuli za Maendeleo. 

Pia amewataka viongozi hao kuwa karibu na wananchi, ili kurahisisha wananchi kufikisha kero zao kwa kwa wakati kabla hawajachukua uamuzi wa kuwatafuta viongozi wa ngazi za juu.

Share To:

Post A Comment: