Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali kabla ya kuzindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya Waziri Simbachawene kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro, mara baada ya Waziri huyo kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiagana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi mara baada ya Waziri huyo kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa na watu wasio wema kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kushikiliwa nchini Dubai.


Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Mtu anaweza kuzusha jambo na likawapotezea muda mwingi wananchi badala ya kufanya mambo ya maendeleo, kwa mfano uzushi kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kuzuiliwa Dubai, nataka niwahakikishie Watanzania kuwa ndege hiyo ipo sehemu husika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 VIP, jijini Dar es Salaam kwenye eneo ambalo Wakala wa Ndege za Serikali wanalitumia na yeyote anayepita barabarani ataiona,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.


Mhe. Simbachawene amesema yeye akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya Utawala Bora ameona aliweke wazi jambo hilo, lililoleta taharuki ili kuwaondoa hofu Watanzania na uvumi huo ulioenea, hivyo lisiwapotezee muda wao na kuwahakikishia wanaovumisha hayo kwa nia ovu wanaweza kwenda kupata uhakika wa uwepo wa ndege hiyo ambapo ameongeza kuwa Viongozi wanasafiri kama kawaida kwa kutumia ndege hiyo.


Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Wajumbe wa Bodi hiyo kushirikiana na Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kuiwezesha Wakala hiyo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


“Ni matarajio yangu kuwa Bodi hii itasimamia vema utendaji wa Wakala hii ili kuleta tija kwa maendeleo ya taifa kama inavyosisitizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro amemuahidi Mhe. Simbachawene kuwa, yeye pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo kwa kushirikiana na Menejimenti ya TGFA watatekeleza yote ambayo ameyaelekeza kwani wanafahamu kwa kina maono makubwa ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika katika kuharakisha maendeleo ya nchi katika kuhakikisha uwepo wa usafiri madhubuti.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi amesema Menejimenti ya Wakala inamhakikishia Mhe. Simbachawene kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu pamoja na maelekezo ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kufikia malengo ya uanzishwaji wa Wakala hiyo.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: