Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mashindano ya Michezo ya ligi ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA yanatarajiwa kuzinduliwa kesho Jumamosi Agosti 26,2023 katika uwanja wa zima moto (fire) Nguzonane mjini Shinyanga.

Mashindano hayo yameandaliwa na umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM kwa kushirikiana na taasisi ya Bega kwa Bega na kwamba timu 32 za mpira wa miguu zitashiriki Mchezo huo utakaofanyika zaidi ya Mwezi mmoja katika Manispaa ya Shinyanga.

Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro amesema uzinduzi huo utakwenda sanjari na zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na jezi kwa kila timu.

Jackline Isaro  amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha michezo.

Amesema mashindano hayo yatatoa fursa na kushirikisha timu mbalimbali zikiwemo timu za taasisi za serikali na taasisi binafsi katika Mkoa wa Shinyanga  kama vile  timu ya SHUWASA, timu za Bodaboda, timu za Masoko pamoja na timu za Walimu.

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan Madete  na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Naibu Katalambula  wamewaomba wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mashindano hayo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fursa za ajira.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Magubika Seleman Amani amesema atahakikisha sheria zote 17 za mpira wa miguu zinazingatiwa huku akiongeza kuwa mashindano hayo ni fursa ya ajira kwa vijana watakao shiriki ambapo amesisitiza timi zitakazo shiriki kuzingatia sheria na taratibu za mpira wa miguu zilizowekwa na TFF.

Bwana Magubika ametaja viwanja 8 vitakavyotumika katika mashindano hayo ikiwemo uwanja wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga, uwanja wa chuo cha ualimu Shinyanga (SHYCOM), uwanja wa kata ya Old Shinyanga, uwanja wa shule ya msingi Kitangili, uwanja wa kata ya Ibadakuli, uwanja wa Jasko kata ya Ngokolo, uwanja wa Ndala shule ya msingi pamoja na uwanja wa Joshoni kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya UVCCM SHY TOWN DR. SAMIA CUP 2023 anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Bi.Mary Pius Chatanda na kwamba kauli mbiu ya mashindano hayo ni SAMIA VIWANJANI.

 

Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro, katikati akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.


Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan Madete  upande wa kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Magubika Seleman Amani katikati akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.

Viongozi mbalimbali 

Viongozi mbalimbali. 

Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: