Mgomo huo umefikia tamati baada ya kudumu kwa siku mbili chanzo kikiwa ni watu wa Daladala kuwalaumu wenzao wa Bajaji kuingilia njia zao na kupandisha abiria kama Daladala.

Akizunguza nasi Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Joseph Michael amesema “Kilichozingatiwa ni Sera, tumewapangia vituo vipya watu wa Bajaji, tunawaondoa Mjini kuwapeleka pembeni na wamekubali hilo.” 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Bajaji Arusha, Shafii Ramadhani amesema “Tumefikia muafaka baada ya kikao na tunashirikiana na Jeshi la Polisi na katika zoezi la vituo vipya lakini Bajaji ambazo zitapata mgawanyo wa vituo ni zile ambazo zimekidhi vigezo vya Leseni na zipo hai.”

Share To:

Post A Comment: