Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa niaba ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu aweso (Mb)ameshiriki kwenye Kongamano la utekelezaji wa Programu ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Zanzibar (Zanzibar Water Investment Programme) ambayo ilizinduliwa mwaka 2022. 

Malengo ya Kongamano ni kukutanisha Wadau wa Sekta ya Maji kujadili na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali pamoja na kutambua maeneo ya ushirikiano.

Kongamano hili limeandaliwa na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Zanzibar kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo; SADC-GMI, pamoja na GWP-TZ ambapo Mgeni Rasmi katika Kongamano hili ni Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.  

Kauli mbiu ya kongomano mwaka huu ni: “Kuongeza kasi ya mabadiliko: katika kufikia usimamizi endelevu wa Rasilimali za Maji chini ya Ardhi pamoja na huduma za uhimilivu kwa wote” "Accelerating change: realizing sustainable management of groundwater resources and resilient water services for all.

" Kauli mbiu nyingine ni: 

Usimamizi wa Maji-Chini ya Ardhi katika Mabadiliko ya Tabianchi (“Groundwater Management in a changing climate”);

Maji-Nishati-Ikolojia ya Chakula na Mazingira (Water, Energy, Food ecosystems, and environment);

Kuimarisha Huduma ya usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira kupitia ubunifu na teknolojia ya Kisasa na Miundombinu (“Enhancing Water Supply and Sanitation through innovative and Climate-Smart Technologies and Infrastructures”);

Usimamizi wa Maji na Uimarishaji wa Taasisi (“Water Governance and Institutional Strengthening”).

Share To:

Post A Comment: