Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameweka mkakatu wa kushirikiana na wadau wa michezo katika kuboresha viwanja vya michezo Jijini Dodoma ili kusaidia Vijana wengi kuwa na sehemu za kuendeleza vipaji vyao kupitia michezo.

Mavunde kayasema hayo jana wakati wa fainali za Ujirani Mwema Mavunde Ndondo Cup 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mtekelezo(Central Secondary School) iliyozikutanisha Timu za Orlando Kaskazini na Majengo Sokoni ambapo Timu ya Majengo sokoni iliibuka bingwa wa mashindano hayo na kuzawadiwa Tsh 5,000,000 ,kombe pamoja na medali.

“ Nizipongeze Timu zote 24 zilizoshiriki katika mashindano haya ambayo yamewakusanya vijana wa kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma.

Naishukuru pia Kampuni ya Mabati ya Taishani kwa kuwa wadhamini wenza wa mashindano haya.

Moja ya mambo makubwa ambayo nitayafanya kwa sasa ni kurekebisha miundombinu ya viwanja vya michezo Jijini Dodoma ili iweze kuchezeka kwa urahisi.

Kwa kuanzia nitaanza na ukarabati wa uwanja huu maarufu wa mtekelezo ambao unawakutanisha watu wengi wa Dodoma kwa kusawazisha sehemu ya kuchezea(_pitch_) na kutafuta wadau ili tuubadilishe uwe wa nyasi pamoja na kuweza uzio”Alisema Mavunde

Wakitoa salamu zao Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wilaya Dodoma (DUFA) Mwl. Joseph Sehaba na Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma(DOREFA) wamempongeza Mbunge Mavunde kwa ufadhili wa mashindano mengi katika Jiji la Dodoma na kuhamasisha michezo kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza katika Fainali hizo,Mmiliki wa Kiwanda cha Mabati cha Taishan Ndg. Andrew Sun amesema Kampuni yake itaendelea kushirikiana na wadau wa michezo Jijini Dodoma ili kukuza na kuendeleza michezo Jijini hapa na kuahidi kuendelea kuwa sehemu ya wadhamini katika mashindano hayo.

Naye Diwani wa Kata ya Uhuru Khalfan Kabwe amempongeza Mbunge Mavunde kwa hamasa kubwa ya michezo katika Jiji la Dodoma na uamuzi wake wa kuboresha uwanja wa Mtekelezo ambao upo ndani ya kata ya Uhuru.






Share To:

Post A Comment: