Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maji , Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso amefungua mafunzo elekezi kwa bodi ya  wakurugenzi RUWASA ambapo yanafanyika Mkoani Iringa 

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Mahundi amesema kuwa kama Wizara wana amini kuwa maadili ya viongozi ni msingi muhimu wa uongozi bora na wenye tija kwa maendeleo endelevu. Hivyo, kwa kusimamia maadili, wajumbe wa bodi mnatakiwa kutekeleza majukumu ya kuiongoza RUWASA. Ni matarajio yangu kwamba mafunzo haya yatawapa mwanga na kuwaimarisha katika kuongoza kwa mfano na kuendeleza maadili "amesema"

Pia,Mhe.Mahundi amesisitiza kwa Wajumbe wa Bodi kuwa wanahitaji kufahama na kusimamia  viashiria hatarishi ili kuhakikisha ustawi na uendelevu wa taasisi. Wajumbe wa Bodi mnahitaji kuwa na ufahamu wa viashiria hatarishi. Hivyo na kusema kuwa  mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutambua, kusimamia, na kupunguza viashiria hatarishi kwa ustawi wa RUWASA

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Bi. Ruth Koya amempongeze Mhe. Rais kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi ya pili ya RUWASA.  Vilevile ameishukuru Wizara ya Maji kwa ushirikiano mzuri wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.


Share To:

Post A Comment: