MBUNGE wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi ameendelea na ziara yake ndani ya Jimbo hilo ambapo amegawa madawati 100 katika Shule ya Msingi Mlimba na Shule ya Msingi Matangini zilizopo kata ya Mlimba. Ambapo kila shule imepata madawati 50.

Akizungumza baada ya kugawa madawati hayo, Kunambi amesema ataendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika jimbo lake kwa kuhakikisha anagusa kila shule lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha elimu.

" Leo nimekabidhi madawati haya 100 ambapo 50 katika Shule ya Msingi Mlimba na 50 Shule ya Msingi Matangini ambapo shule hizi zote zilikua na uhaba mkubwa wa madawati. Najua zipo changamoto zingine pia niwaahidi nimezibeba ntashughulika nazo.

Serikali yetu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kubwa ya kuwapatia elimu bila malipo watoto wetu, hivyo ni wajibu wetu kama wasaidizi wake kumuunga mkono katika azma yake hii ya kuhakikisha kiwango cha elimu kinakua. Tumeanza na madawati lakini ni ahadi yangu kwenu kwamba tutagusa kila eneo," Amesema Kunambi.

Wanafunzi wa Shule zote mbili wametoa shukrani zao kwa Mbunge Kunambi na kumuahidi kuyatunza madawati hayo ili pia yaweze kudumu na kutumiwa na wenzao wa baadaye huku wakimuahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao.

Share To:

Post A Comment: