Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mh. Gekul Pauline ambaye pia ni mbunge wa Babati mjini amefanya kikao cha utatuzi wa mgogoro wa kikatiba uliodumu kwa muda mrefu ndani ya kanisa la Elim Pentekoste leo jijini Dodoma.
Kikao hicho kiliketi jijini Dodoma kwa muda wa masaa 15 tangu sa tano asubuhi hadi sa nane usiku baina ya pande mbili zinazosigana ndani ya kanisa hilo wakilalamikia uvunjivu wa katiba yao ya kanisa.
Habari njema ni kwamba pande hizo zote mbili zimekubali kusameheana na kuanza upya mchakato wa katiba ya kanisa lao ambayo ina mapungufu mengi hivyo kusababidha migogoro ndani ya kanisa.
Wachungaji hao , maaskofu na askofu mkuu wa kanisa hilo ambao wametoka mikoa mbali mbali hapa nchini wamekubali kwa pamoja kusameheana na kuanza upya kwa marekebisho ya katiba yao ambayo ndio ilikuwa chanzo kikubwa cha mpasuko huo ndani ya kanisa hilo.
Share To:

Post A Comment: