Na Moreen Rojas,Dodoma.

Ndani ya mwaka wafedha 2022/23 DAWASA imeweza kutekeleza jumla ya miradi 10 ya kimkakati na zaidi ya miradi midogo midogo 86 ya kusogeza huduma kwa wananchi.


Hayo yameelezwa na Kiula Kingu Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam(DAWASA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelezea mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha2023/24.


Aidha amesema kuwa miradi hii ilihusisha kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa, kujenga matenki makuu ya kuhifadhi maji, kujenga vituo vya kusukuma maji nakuongeza mtandao wa mabomba ya maji ili maji yanayozalishwa yaaweze kufikia wananchi ndani ya eneo la huduma.


"Miradi mikubwa iliyo tekelezwa na kukamilishwa 2022/23 ni pamoja na,mradi wa ujenzi wa mfumowa usamabzaji maji kati ya Bagamoyo hadimatenki yaliyopo jirani na Chuo kikuucha Ardhi, mradi wa maji Kigamboni, mradi wa maji Chalinze awamu ya tatu, mradi wa maji Mshikamano, mradi wa maji nje ya mtandao(unaohudumia mitaa 12), mradi wa Maji Mbezi Makabe,mradi wa maji Zegereni, Mradi wa maji Soga, Mradi wa maji Mbwawana miradi ya maji 14 iliyotekelezwa chini ya programu ya lipa kwamatokeo. Miradi hii ambayo ina uweo wa kuhudumia wakazi 722,308 katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani ilijengwa kwa gharama ya jumla shilingbilioni219.4"Amesema Kingu.


Aidha ameongeza kuwa Mwaka wa fedha 2023/2024, DAWASA imejipangakuendeleakuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati saba ikiwemo Mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, Mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji, Mradi wa maji Kwala, Mradi wa maji Mji wa Pangani Kibaha, Ujenzi wa mradi kutoka Kimbiji-Kigambonihadi jirani naChuo cha Uhasibu T.I.A, Ujenzi wa mradi wa maji Kusini mwa Jiji la Dar es salaamna Mradi wa uchimbaji visima virefu tisa eneo la Kigamboni.


"Miradi hii itakayotekelezwa kwa jumla ya Tsh.Bilioni 425.9 ina inalenga katika; kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA,kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji, kuimarisha mfumo wa usambazaji majina kuimarisha huduma katika maeneo ambayo hayana mtandao hasayale ya pembezoni".


Utekelezaji wa Miradi ya Usafi wa Mazingira kuboresha afya na mazingira Pamoja na kuwekeza nguvu katika utoaji wa huduma za majisafi, DAWASA imejipanga kikamilifu nakuchukua hatua za makusudi za kuboresha usafi wa mazingira kupitia miradi mikubwa na midogo. 

Hii ni kwasababu upatikanaji wa maji unapoongezeka unapaswa uambatane na usimamizi madhubuti wa usafi wa mazingira.

Katika Wilayaya Kinondonina Ilala, miradi ya kuchakata majitaka itajengwa maeneo ya Mbezi Beach na Buguruni  Mradi wa Mbezi Beach unatekelezwa kwaushirikiano kati ya Serikali na Benki ya Duniaambapo jumla ya shilingi bilioni 132.3 zitatumika kujenga mtambo wa kisasa wenye uwezo wa kuchakata lita milioni 16 kwasiku. 

Aidha mradi meingine ni wa kujenga mfumo wa kukusanya majitaka na maeneo nufaika katika awamu hii ni Mbezi beach, Kilongamwima, baadhi ya maeneo ya Kawe na Salasala. 

Utekelezaji wa mradiumeanza na Wakandarasi wanaendeleana shughuli za maandalizi ya ujenzi. 

DAWASA pia imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo ya kuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi yalita 780,000 za majitaka zitakuwa zikichakatwa kwa siku.

Miradi hiiambayo pia itajumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30, itasaidia kuongeza wigo waupatikanaji wa huduma hizi muhimu na hivyo kuboresha usafi wa mazingira. Aidha miradi hiiitasaidia wananchi kupata huduma za usafi wa mazingira kwa gharama nafuu karibu na maeneo wanayoishi. 

Wakandarasi wanaotekeleza miradi wanaendelea na ujenzi. Gharama za miradi hii ni jumla yaTsh.bilioni 25.7na wanufaika wa miradi hii wanakadiriwa kufikia milioni1.8 


Miradi hii ni ya kisasa na katika mfumo wake wa uchakatajimajitakaitatoa gesi asilia kwa ajili ya kupikia, itatoa mbolea itakayoweza kutumika katika kustawisha bustani za miti na majani lakini pia maji yatakayochakatwa yataweza kutumika kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji, usafishaji wa barabara na mitaro ama kupoozea mitambo.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: